MKUU wa Mkoa wa Mwanza, Amos Makalla amezitaka halmashauri ambazo bado hazijafanya vizuri katika zoezi la kutoa chakula shuleni kwa wanafunzi kuendelea na ushawishi kwa wazazi au walezi kuona umuhimu wa kuchangia zoezi hilo kwani ni jambo ambalo lina umuhimu kwa kipindi chote cha wanafunzi wawapo shuleni.
Makalla amesema hayo jana alipokutana na watendaji mbalimbali wa serikali katika Mkoa wa Mwanza kwenye kikao cha tathimini ya utekelezaji wa mkataba wa lishe kwa kipindi cha Julai 2022-2023 kilichofanyika kwenye ukumbi wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa .
Amesema halmashauri ambazo bado hazijafanya vizuri katika zoezi hilo ni pamoja na Magu ambao wamefanikiwa kutoa chakula kwa wanafunzi kwa asilimia 47,Buchosa 47,Ukerewe 51,Sengerema 51 na Halmashauri ya Jiji la Mwanza 67.
Amesema halmashauri ambazo zinaendelea kufanya vizuri katika zoezi la kutoa chakula kwa wanafunzi ni pamoja na Ilemela, Misungwi na Kwimba
“Nitoe taadhari kigezo cha mtoto kutochanga au kuwa nanmchango wa chakula shuleni isiwe kigezo cha kumrudisha na kukosa masomo bali tuwashawishi wazazi na walezi waone umuhimu wa kuchangia chakula kwa kwanafunzi kwa kipindi chote cha masomo.” Amesema Makalla.
Amesema kuwa Serikali inaweka msukumo wa pekee kwenye masuala ya lishe kwani wakuu wa mikoa wamesaini mkataba na Rais wa Jamuhuri ya muungano wa Tanzania kuhusu maeneo maalumu ya kuweka mkazo katika suala la lishe.
Kwa upande wake mmoja wa maofisa lishe wa Mkoa wa Mwanza Sophia Lazaro amewaomba wakurugenzi kuziwezesha halmashauri zao pamoja na maafisa lishe ili waweze kutekeleza majukumu yao kwa ufanisi zaidi ikiwa.
Comments are closed.