RC Pwani ataka weledi kwa watendaji

PWANI: Mkuu wa Mkoa wa Pwani, Abubakar Kunenge, amesema wakuu wa wilaya, wakurugenzi na watendaji mbalimbali wa serikali wanapaswa kuhakikisha wanatekeleza majukumu yao kwa wakati na kwa kuzingatia kanuni na taratibu ili kuondoa urasimu unaochelewesha huduma kwa wananchi na kukwamisha wawekezaji.
Kunenge ametoa kauli hiyo leo Desemba 11, 2025 mjini Kibaha katika kikao kazi cha kutathmini utekelezaji wa ahadi za Rais Dk Samia Suluhu Hassan ndani ya siku 100 tangu aingie madarakani, ambapo amesisitiza umuhimu wa uwajibikaji katika ngazi zote za mkoa, wilaya na halmashauri.

Amesema licha ya changamoto ya kupungua kwa misaada ambapo kwa mwaka huu wa fedha misaada inakadiriwa kufikia asilimia 1.9 tu, mkoa unajipanga kuhakikisha miradi ya maendeleo inaendelea kutekelezwa kwa kuongeza mapato ya ndani, matumizi mazuri ya rasilimali na kuimarisha ukusanyaji wa mapato.

Aidha, Kunenge ameonya kuwa urasimu unapunguza ufanisi, hivyo watendaji wanapaswa kufanya kazi kitaalamu na kwa uwajibikaji ili kufikia malengo yaliyowekwa na mkoa pamoja na serikali kuu.
Amesema mkoa utaendelea kuchukua hatua za kimkakati katika maeneo yote yanayohusu utoaji wa huduma kwa wananchi na mazingira bora ya uwekezaji



