KAIMU Mkuu wa Mkoa wa Katavi, ambaye ni Mkuu wa Mkoa wa Rukwa, Queen Sendiga amepongeza usimamizi wa ujenzi wa miradi ya vyumba vya madarasa katika shule za Sekondari Lyamba, Mpanda Day na Misunkumilo, Halmashauri ya Manispaa ya Mpanda.
Alitoa kauli hiyo katika ziara yake ya kukagua miradi hiyo na kutoa wito kwa wasimamizi kuhakikisha wanaisimamia vizuri hadi mwisho.
Kwa upande wake Meya Manispaa ya Mpanda, Haidary Sumry alimshukuru Mkuu wa Mkoa, Mkuu wa Wilaya ya Mpanda na viongozi wengine kwa namna ambavyo wamekuwa wakipita kukagua miradi mara kwa mara, jambo linaloongeza umakini na kuisimamia ipasavyo.