RC Shinyanga aipongeza halmashauri kujibu hoja

MKUU wa Mkoa wa Shinyanga, Christina Mndeme ameipongeza Halmashauri ya Msalala wilayani Kahama kwa kuendelea kujibu hoja 59 mkaguzi zikijumulisha hoja za nyuma huku wakiendelea kuongeza juhudi za ukusanyaji wa mapato.

Mndeme aliyasema hayo jana kwenye kikao cha baraza maalum la kujibu hoja za mkaguzi katika hiyo ambapo aliwaeleza wahakikishe kuzingatia sheria na miongozo ili kuweza kujibu hoja zote.

Mndeme alisema kati ya hizo hoja 59 hoja 28 zimefungwa, hoja 31 bado zinaendelea kutekelezwa hivyo alipongeza ukusanyaji wa mapato kufikia asilimia 102 nakufikisha lengo kabla ya mwaka wa fedha 2022/2023 kuisha.

Advertisement

Mndeme alisema halmashauri hiyo imeweza kupata hati safi kwa kipindi cha miaka miwili mfululizo isipokuwa mwaka 2020 waliipata hati yenye mashaka na juhudi hizi zinatokana na maelewano mazuri kwa watalaamu na madiwani.

“Masuala ya kuzingatia na ushauri umetolewa na Mkaguzi kuhakikisha Fedha zinazokusanywa kwa njia ya mashine za Kielektroniki (POS) zipelekwe Benki kwa wakati,kuzingatia taratibu na kanuni za manunuzi na Ushuru wa huduma sanjari na maeneo ya halmashauri kupimwa”alisema Mndeme.

Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu Hesabu za Serikali (CAG) Mkoa wa Shinyanga Shinyanga, Patrick Lugisi alisema halmashauri hiyo imefanya vizuri kujibu hoja 59 zikijumulisha hoja za nyuma na bado hoja 31 zinaendelea kutekelezwa .

Makamu mwenyekiti wa halmashauri hiyo Flora Sagasaga alisema maoni na ushauri wa mkaguzi waliapokea na hoja ambazo zinasumbua ziko nje ya uwezo wao mfano za mgawanyo wa Mali na upimaji wa maeneo kukosekana nyaraka muhimu za umiliki lakini zingine tayari zimefanyiwa kazi.

muweka hazina wa halmashauri hiyo Godon Julias alisema hoja ambazo hazikufungwa zimetokana na maeneo yaliyojengwa majengo ya taasisi kutokuwa na hati miliki nakukosekana uhalali wa umiliki na sh Millioni 115.7 kutopelekwa Benki nakukosa vielelezo.

Mkurugenzi wa halmashauri hiyo khamis Katimba alisema amekuja muda mfupi lakini Mahusiano ameyaona wataendelea kutekeleza ahadi ya chama na sera ya serikali kuwapatia huduma wananchi.

1 comments

Comments are closed.

/* */