MKUU wa Mkoa wa Shinyanga, Annamringi Macha amesema viongozi waliochaguliwa kama watakwenda kinyume na utaratibu serikali haitosita kuwaondoa na kuwataka waondoe changamoto ya kutosoma mapato na matumizi kwenye maeneo yao.
Macha amesema hayo leo kwenye mkutano maalumu wa kuapishwa viongozi waliochaguliwa wa serikali ya Mitaa kwa viongozi Mtaa,vitongoji na vijiji huku akiwataka wakurugenzi wa halmashauri sita za mkoa huu kuwapatia mafunzo ya uwajibikaji.
Macha amesema moja ya jambo ambalo wamekuwa wakilalamikiwa viongozi wa serikali za mitaa ni kutosoma mapato na matumizi pia uchaguzi wa serikali za mtaa umekwisha hivyo wawe na umoja wa kushirikiana katika kazi ili wawatumikie wananchi.
“Jambo la kwanza ninalo taka liwepo ni kuhakikisha kunakuwepo amani kwenye maeneo yenu kwani bila amani hakuna uongozi katika serikali na kila mmoja apate miongozo ya nakala ya kusoma ili muweze kufanya rejea katika kazi zenu,” amesema Macha.
Macha amewataka viongozi hao washirikishe na vyombo vya usalama katika ulinzi na kuwatambua wananchi kwenye maeneo wanayowaongoza ili kuwafahamu wanafanya shughuli gani pia.
Macha amesema kila mtaa,vitongoji na vijiji kuna shughuli au miradi zinazofanywa hivyo wahakikishe wanakuwa walinzi wa miradi iliyotekelezwa au inayoendelea mfano ujenzi wa shule au zahanati.
“Ninyi viongozi mhakikishe mnalinda migogoro ya ardhi na kuiepuka kwani ilikuwepo changamoto ya muingiliano kati ya mtendaji au mwenyekiti kila mmoja anamajukumu yake hivyo mshirilishane na kupeana majukumu”amesema Macha.
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa Shinyanga Alexius Kagunze amesema kulikuwa na mitaa 57,Vijiji 17 na Vitongoji 84 na maeneo karibu yote wamepita Chama Cha Mapinduzi ilisipokuwa kitongoji kimoja ndiyo ameshinda aliyekuwa mgombea wa Chadema.
Mwenyekiti wa Mtaa wa Majengo Issa Mkondo na Mwenyekiti wa Mtaa Bugweto A, Mary Makamba wamesema suala la ulinzi na usalama na kuhakikisha kutojipatia fedha kwa njia isiyohalali na kuwatumikia wananchi shida zao.
“Katika kipindi cha miaka mitatu ya uongozi wangu tutahakikisha tunarejea, kuandaa mitaala pamoja kuongeza program za masomo zinazojibu changamoto mbalimbali katika sekta ya mazingira maliasili na utalii na pia kukifanya chuo kukubalika kama chuo mahiri cha kutoa mafunzo katika taaluma mbalimbali za uhifadhi, maliasili na utalii na hili tunalenga hasa nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) na nchi wanachana wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika( SADC)” amefafanua Prof. Mgaya.
Uzinduzi huo umehudhuriwa na mkuu wa chuo hicho na Katibu wa Bodi, Prof. Jafari Ramadhani kideghesho, wajumbe wa bodi, uongozi wa chuo na viongozi wa serikali ya wanafunzi.