Real Madrid vs Pachuca: Fainali mabara leo

Wachezaji wa kikosi cha Real Madrid wakifanya mazoezi.

FAINALI ya Kombe la Mabara la FIFA 2024 kati ya Real Madrid ya Hispania na C.F. Pachuca ya Mexico inapigwa leo kwenye uwanja wa Lusail uliopo mji wa Lusail, Qatar.

Awali michuano hiyo ilijulikana kama Kombe la Dunia la Klabu.

Real Madrid ilijihakikishia nafasi katika fainali hiyo tangu Juni 1 ilipotwaa ubingwa wa Ligi ya Mabingwa Ulaya kwa kuizamisha Borussia Dortmund kwa mabao 2-0 kwenye uwanja wa Wembley, London.

Advertisement

Pachuca imetinga fainali baada ya kuitoa Al Ahly kupitia mikwaju ya penalti 6-5.