REST yachochea mabadiliko jumuishi kwa watu wenye ulemavu

IRINGA: KATIKA taifa linalojivunia misingi ya usawa na haki kwa wote, bado kuna maswali mengi kuhusu nafasi ya watu wenye ulemavu katika maendeleo ya jamii.
Mwenyekiti wa Chama cha Watu Wenye Ulemavu Mkoa wa Iringa, Shabani Shomari anasema; “Hili ndilo linalojitokeza wazi mkoani Iringa, ambako kwa muda mrefu kundi hili limekuwa likikabiliwa na changamoto za kijamii, kiuchumi na kimfumo.”
Lakini sasa, anasema hali hiyo inaonekana kubadilika—shukrani kwa mradi wa Reproductive Equity Strategy in Tanzania (REST).
Kwa kushirikiana na serikali na mashirika ya kiraia, Shirika la DSW Tanzania limeanzisha mradi huo wa REST, ambao pamoja na mambo mengine unalenga kuwajengea uwezo watu wenye ulemavu kushiriki kikamilifu katika shughuli za kijamii, kisiasa na kiuchumi.
Ni hatua inayotajwa kuwa ya kihistoria, ikilenga kuvunja minyororo ya ubaguzi wa muda mrefu na kuwawezesha watu hawa kuwa sehemu hai ya maendeleo ya taifa.
Mratibu wa Mradi huo kutoka DSW Tanzania, Celina Protas, anasema mradi huo unakwenda mbali zaidi ya kutoa elimu; unawajengea watu ujasiri wa kudai nafasi zao katika jamii na kuchukua hatua za kuleta mabadiliko.
Katika mafunzo kwa walemavu yaliyofanyika mjini Iringa na kushirikisha asasi za kiraia zaidi ya 10 zinazofanya kazi na DSW Tanzania, Protas alisema REST inalenga pia kuamsha ari ya ushiriki wa watu wenye ulemavu katika mchakato wa uchaguzi mkuu ujao na katika nafasi nyingine za uongozi.
“Walemavu si watu wa huruma. Ni rasilimali ya Taifa, tunapowatenga, tunapoteza nguvu ya pamoja ya maendeleo,” anasema.
Alisema mafunzo hayo yameshirikisha watu wenye ulemavu wa aina mbalimbali ukiwemo wa viungo na usikivu, lengo kuu ni kuwawezesha kushiriki kwa ujasiri katika mchakato wa maamuzi, kutangaza haki zao na kujikwamua kiuchumi.
Kwa mujibu wa takwimu za Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS), ni idadi ndogo tu ya watu wenye ulemavu wanaoshiriki katika shughuli rasmi za maendeleo kutokana na changamoto kama ukosefu wa miundombinu rafiki, mitazamo hasi na elimu duni kuhusu haki zao.
Afisa Maendeleo ya Jamii wa Mkoa wa Iringa, Fatuma Mohamed, anasema mitazamo ya kibaguzi bado ni kikwazo kikubwa.
“Tunapaswa kuondokana na dhana ya kuwaona watu hawa kama mzigo. Wanahitaji fursa, si huruma,” anasisitiza.
Mkurugenzi wa shirika linalojihusisha na maendeleo ya viziwi mkoani Arusha (DCPO), Ramadhani Hamisi anaeleza kuwa kuja kwa mradi wa REST kumewafanya watu wenye ulemavu wajione kuwa sehemu ya mfumo rasmi wa Taifa.
“Mradi huu umetuletea mwamko mpya wa matumaini. Tunaamini tunaweza kushiriki kikamilifu kama wengine,” alisema.
REST imeahidi kuendelea na kazi hiyo hata baada ya mafunzo kwa kufuatilia utekelezaji wa sera na sheria zinazolinda haki za watu wenye ulemavu, ili kuhakikisha kuwa wanapewa fursa sawa kama wengine katika jamii.
Katika safari ya kuelekea utekelezaji wa Ajenda ya Maendeleo Endelevu (SDGs), Tanzania haina budi kuhakikisha kuwa hakuna anayeachwa nyuma—na REST ni sehemu ya jibu la msingi kwa hilo.
Mkurugenzi wa miradi kutoka shirika la Tahea linalofanya kazi na DSW Tanzania kupitia mradi huo Peter Mapunda alitoa wito kwa serikali, sekta binafsi na jamii kwa ujumla kuondoa vikwazo vya kimtazamo na kimazingira vinavyowazuia watu wenye ulemavu kushiriki kikamilifu katika maendeleo ya taifa.
Thank you for the good writeup. It in fact was a amusement account it.
Look advanced to more added agreeable from you!
However, how could we communicate?
buy viagra online