Ripoti yafichua rushwa ya ngono inavyowaathiri wanahabari wanawake

RIPOTI ya Haki za Binadamu na Biashara ya mwaka 2021/2022 iliyozinduliwa leo Ijumaa, jijini Dar es Salaam imeonesha kuwa rushwa ya ngono kwa waandishi wa habari wanawake ni janga kubwa linalowakawamisha katika tasnia hiyo.

Afisa Programu Mwandamizi Masuala Biashara na Haki za Binadamu kutoka Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC), Joyce Komanya amesema asilimia ya wanawake waliohojiwa walisema hali ya rushwa ya ngono ni mbaya.

Komanya amesema wengine asilimia 40 walisema ni mbaya lakini kawaida, asilimia 4 walisema ni mbaya na waliwahi kushuhudia na asilimia zaidi ya 10 walisema hawajui.

Advertisement

“Changamoto kubwa ambayo waandishi wa habari wanawake waliielezea walisema ni rushwa ya ngono na walivyozungumzia rushwa ya ngono; tuliwauliza hii changamoto ni kubwa kiasi gani ni mbaya sana, ni mbaya kiasi, ni kawaida au hakuna kabisa.

Amesema rushwa ya ngono ina athari kimwili, kiakili huku akitolea mfano mfanyakazi anayekwenda ofisini kila siku na bosi anamfanyia matendo hayo hawezi kufanya kazi vizuri hivyo hata utendaji kazi unaathirika.

“Haki zingine zinakiukwa kutokana na rushwa ya ngono mtu amekataa kutembea na bosi wake anafukuzwa kazi au halipwi mshahara au anapewa nafasi fulani ambayo amesoma na kuna nafasi anatakiwa apate lakini kwa sababu amekataa kutembea na bosi hapati,” ameeleza Komanya.

/* */