RSF wako tayari kuleta amani Sudan

KIKOSI cha Msaada wa Haraka cha Sudan (RSF) kimesema kipo tayari kusimamisha mapigano mara moja bila masharti kupitia mazungumzo na jeshi la Sudan huku kikitia saini tamko na muungano wa kiraia wa Taqadum na kulitaka jeshi kufanya hivyo.


Juhudi za kumaliza mzozo huo kupitia mazungumzo yanayoongozwa na Marekani na Saudi Arabia hadi sasa hazijafua dafu na makubaliano ya awali ya kuwalinda raia hayajazingatiwa.

Kwa kutia saini kile kiitwacho Azimio la Addis Ababa, ambalo linakusudiwa kutumika kama msingi wa mazungumzo zaidi na suluhu ya kisiasa, RSF imeonesha dhamira ya wazi kumaliza vita.

Huku RSF, ambayo inashutumiwa na U.S. kwa uhalifu dhidi ya ubinadamu, ikipata nguvu katika wiki za hivi karibuni, haijulikani ni kwa kiasi gani aliyekuwa Naibu Mwenyekiti wa Baraza la Mpito la Uhuru wa Sudan, Dagalo atatekeleza ahadi za tamko hilo.

Habari Zifananazo

Back to top button