Ruge: Mama unaupiga mwingi

KATIBU wa  Baraza la Wanawake Chadema Taifa, (BAWACHA), Catherine Ruge amesema Rais Samia Suluhu Hassan anaupiga mwingi katika kutekeleza miradi mbali mbali ya maendeleo na kuboresha demokrasia nchini.

Ruge ameyasema hayo leo Machi 8, 2023 katika kilele cha maadhimisho ya siku ya wanawake duniani, ambapo Bawacha wameadhimisha katika ukumbi wa Kuringe mjini Moshi.

Amesema “Rais Samia Suluhu, naomba utambue kuwa hatujakualika kwa bahati mbaya, haya sio maadhimisho ya wanawake wa Chadema, bali ni maadhimisho ya wanawake wote ikiweo wewe mheshimiwa Rais.

“Mhe. Rais naomba nikukumbushe kuwa kwa mujibu wa sensa wanawake ni jeshi kubwa tuko milioni 31, ukubwa huu sio tu kwa idadi lakini pia kwa kuchangia kulipa kodi, inawezekana wanawake wa CCM hawakwambii ukweli au kukwambia kuwa mama unaupiga mwingi sana.

“Leo tutakueleza mambo mengi ambayo mengine haujawhai kusikia lakini leo utapata fursa ya kuyasikia, tunatambua mheshimiwa Rais unafanya jitihada kubwa sana kwa kushirikiana na mwenyekiti wetu Freeman Mbowe kuhakikisha tunapata katiba mpya na tume huru ya uchaguzi kabla yam waka 2025

Aidha, Ruge amesema idadi ya vifo vya wanawake na watoto bado iko juu, kwa mujibu wa takwimu za Benki ya Dunia zinasema katika kila watoto 1000, watoto 30 hufariki na asilimia 64 ya watoto wanaofariki ni watoto wachanga

“Hatufurahishwi na mauaji katika maeneo mbali mbali yanayofanywa na jeshi la Polisi, tutaendelea kutetea haki zote ikiwemo haki ya kuishi. Tuko tayari kushirikiana nawe Rais na yeyote katika kutetea haki.

Habari Zifananazo

Back to top button