‘Rumbesa chanzo kipato kushuka’

KIBAHA, Pwani: WAKALA wa vipimo mkoani Pwani, imewaonya wafanyabishara kuacha mara moja tabia ya kuendelea kuvunja sheria kwa kutumia vipimo visivyo rasmi ikiwemo rumbesa hatua ambayo itasaidia kuongeza Mapato yao na kuimarisha uchumi wao na taifa kwa ujumla.

Hayo yalibainishwa na Kaimu Meneja wa wakala wa vipimo mkoani hapa, Hashimu Athuman, wakati akizungumza na wafanyabishara Soko la Loliondo wilayani Kibaha na Bagamoyo, ikiwa ni sehemu ya kuhazimisha sikukuu ya vipimo duniani  iliyobebwa na kauli  mbiu ya “tupime leo kwa ajili ya kesho endelevu”.

Amesema licha ya serikali kutoa elimu na kuwekwa kwa sheria ya vipimo nchini bado baadhi ya wafanyabishara ambao sio waaminifu wamekuwa wakitumia vipimo visivyo rasmi jambo ambalo ni kinyume na sheria na kwamba serikali haita sita kuwachukulia hatua.

Soma pia: https://www.instagram.com/p/C7MZWh_u21M/?utm_source=ig_web_copy_link&igsh=MzRlODBiNWFlZA==

“Wafanyabiashara mmekuwa mkitumia visado,ndoo na rumbesa jambo hili halitakiwi ni kinyume cha sheria na mkitumia vipimo hivi mnaweza mkawa mnajipunja  wenyewe hivyo mnapaswa kuzingatia sheria mtumie mizani jambo hili litasaidia kuongeza Maputo yenu na ya taifa pia,”amesema.

Amesema iwapo wafanyabishara watazingatia na kufuata sheria kwa kutumia mizani kupima bidhaa za mazao mashambani itasaidia kuongeza kushindani wa masoko ya Nje ya nchi tofauti na ilivyo kwa sasa.

Ameeleza kuwa wakala wa vipimo, wanaendelea kutoa elimu  ya matumizi sahihi ya vipimo vilivyopo kisheria  ikiwemo kufanya utafiti juu yachangamoto zinazo wakabili wafanyabishara kuhusiana sekta hiyo, hatua ambayo itasaidia kuondoa kero na malalamiko mbalimbali.

Soma pia: https://habarileo.co.tz/wafanyabiashara-washauriwa-kuweka-nembo/

Wakizungumza kwa nyakati tofauti baadhi ya wafanyabishara hao walisema, wamekuwa wakikabiliana na changamoto nyingi ikiwemo wakulima kushindwa kutumia vipimo sahihi kuanzia shambani jambo ambapo elimu inapaswa kuanzishi vijiji badala ya kuwabana wafanyabishara mini.

“Tunapoenda shamba kununua mazao wakulima hatumii mizani hivyo sisi pia tunapofikisha bidhaa sokoni hatuwe kutumia mizani kwa kuhofia kupoteza mitaji yetu hivyo nitake wakala  wa vipimo elimu ianzie vijijini kule kwa wakulima,” amesema Ally Pazi.

Naye, Yusuph Msuya ,alisema bado elimu ya vipo inapaswa kutolewa badala ya kuendelea kuwatoza faini wafanyabishara jambo ambalo limekuwa likiumiza biashara zao na kuishia kufilisika.

Habari Zifananazo

Back to top button