NCHI za Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Jangwa la Afrika (SADC) na Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) zimetakiwa kuainisha mikakati ya kitaifa na kikanda ikiwemo kutumia usaidizi wa kifedha katika kutekeleza miradi mikubwa yenye matokeo yenye matokeo ya muda mrefu.
Aidha ameagiza kuwekeza katika utafiti,maendeleo na kuimarisha uwezo wa uzalishaji wa ndani ili kuhakikisha teknolojia za ufanisi wa nishati zinapatikana, zinaweza kununuliwa na kufaa kwa mahitaji ya kipekee ya jumuiya hizo.
Hayo yamesemwa Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dk, Doto Biteko jijini Arusha wakati wa kufungua Mkutano wa Kikanda wa Masuala ya Matumizi Bora ya Nishati (Regional Energy Efficiency Conference – REEC), wenye Kauli Mbiu ya Mkutano ni “Kuchagiza Matumizi Bora ya Nishati kwa Maendeleo Endelevu”
Amesema endapo SADC na EAC zikianisha mikakati ya pamoja na kupata usaidizi wa kifedha kutekeleza miradi mikubwa wataweza kupata nishati ya kuaminika, kupunguza uzalisha wa gesi chafu na kukuza ukuaji endelevu wa uchumi.
Katika COP28, serikali zilijitolea kuongeza maradufu kiwango cha wastani cha kimataifa cha kila mwaka cha uboreshaji wa ufanisi wa nishati ifikapo 2030 ambapo Wakala wa Kimataifa wa Nishati (IEA) wanaonyesha kuwa maendeleo ya nishati safi kila mwaka yanahitaji kuongezeka kutoka asilimia 2 ya sasa hadi zaidi ya asilimia 4