Safari za ndege kati ya India na China kuanza rasmi

INDIA : SERIKALI ya India na China zimekubaliana kuanzisha safari za ndege za moja kwa moja za abiria kati ya nchi hizo mbili.

Uamuzi huu umefikiwa baada ya nchi hizo mbili kuendelea kuwa na uhusiano wa karibu katika kipindi cha miaka mitano sasa.

Safari za ndege za abiria kati ya India na China zilisitishwa mwanzoni mwa janga la UVIKO-19.

Hata hivyo, baada ya janga la UVIKO =19 kupita safari hizo hazikuweza kuanza kufuatia kuzorota kwa uhusiano kati ya Beijing na New Delhi.

Mvutano ulipamba moto mnamo 2020 kufuatia mapigano ya kijeshi kwenye mpaka unaozozaniwa huko Himalaya na kuifanya India kusitisha rasmi safari za ndege za abiria kuelekea China.

Hapo awali, karibu safari 500 za moja kwa moja kila mwezi kati ya China na India zilifanyika kabla ya janga la UVIKO-19. SOMA: India yazungumzia amani, usalama BRICS

Kwa sasa uhusiano kati ya nchi hizi mbili umeimarika kufuatia mikutano ya ngazi ya juu, yakiwemo mazungumzo kati ya Rais wa China Xi Jinping na Waziri Mkuu wa India Narendra Modi nchini Urusi mwezi Oktoba.

Habari Zifananazo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button