Sakata la anayedai kubadilishiwa namba latua NECTA

BARAZA la Mitihani nchini (NECTA), limesema linafanyia kazi taarifa iliyosambaa mitandaoni ikimuonesha mtahiniwa Iptisum Suleiman Slim akilalamika akidai kubadilishiwa namba yake ya mtihani wa darasa la saba.

Mwanafunzi huyo wa shule ya Chalinze Modem Islamic Pre&Primary School, amelalamika katika video fupi iliyosambaa mtandaoni, akidai kubadilishiwa namba yake ya mtihani wa darasa la saba uliofanyika Oktoba 5 na 6, 2022.

“Baraza la mitihani linaifanyia kazi taarifa hiyo kuhakikisha mtahiniwa huyo anapata haki yake,” amesema Ofisa Uhusiano wa NECTA, John Nchimbi.

 

Habari Zifananazo

1 Comment
Oldest
Newest Most Voted
Inline Feedbacks
View all comments
Back to top button