Sakata la DP World Kinana ataka utulivu

Asema, hofu, hoja zinazotolewa zitafanyiwa kazi na serikali

WAKATI  hoja mbalimbali zikiendelea kutolewa kuhusu mkataba wa uendelezaji na uboreshaji wa bandari baina ya Tanzania na Dubai, Chama Cha Mapinduzi (CCM) kimewataka wananchi kuwa watulivu, kwa kuwa hoja na hofu zao zinashughukiwa na serikali
Hayo yamesemwa leo jioni  Julai 26,2023  na Makamu Mwenyekiti wa  CCM Bara,  Abdulrahman Kinana katika mkutano wa hadhara uliofanyika katika Uwanja wa Mkendo, uliopo Musoma Mjini mkoani Mara.
Amesema, Rais Samia amekaa kimya kwa muda wote hajaongea chochote ni kwamba bado serikali inapokea maoni yanayotolewa na watu mbali mbali na yatafanyiwa kazi.
“Rais ambae amekula kiapo, eti atafanya jambo ambalo  halina maslahi na nchi, haiwezi kutokea. ” Amesema na kuongeza
 ” Kama Rais tangu amechukua usukani amefanya yote aliyoyafanya akauze bandari sababu ni ipi? ili iweje? ukisikiliza mjadala wote tunaotetea, wanaopinga, wanaokosoa hakuna anaesema kusiwe na uwekezaji hata mmoja, wote wanakubali kuna haja ya kuwekeza, na lengo ni moja kuongeza ufanisi na kuongeza mapato.
“Serikali imesema hivi tunaenda kufanya uwekezaji kwa nia njema ya kuleta ufanisi, kuongeza mapato ili tuweze kufanya shughuli nyingi za maendeleo, “amesema.
Amesema, wamejitokeza watu wameanza kuhoji, wapo wanaohoji kwa nia njema ya uzalendo wapo, hawawezi  kusema kila anayehoji ana nia mbaya, wapo wanaopitia mkataba wametoa ushauri mzuri, serikali imesema hivi itapokea itapokea kila ushauri unaotolewa.
“Chama chetu  na serikali isikilize maoni na ushauri wa wananchi, inasikiliza hoja inayotolewa na inasikiliza pia hofu inayotolewa,haya yote yatafanyiwa kazi, haiwezekani Rais akapuuza yote haya.” Amesema
Amesema,  Rais amekaa kimya tangu mjadala umeanza kwa kuwa kiongozi mzuri yanapotokea mambo ambayo kuna ubishi na mabishano, na hoja mbalimbali sio yule anaejaribu kujibu kila hoja, kiongozi mzuri ni yule aliyetulia, anachofanya Rais ni kutulia, kusikiliza kila hoja, kuchambua kila hoja, kutathimini kila hoja ili muda ukifika, upatikane  uwekezaji uliobora zaidi kwa manufaa ya Watanzania.
Amesema, “tupo watu wengi, vyama vingi, kupiga kelele imeuzwa imeuzwa, kwa nini iuzwe, ili iwe vipi, naomba tuwe watulivu tumuamini Rais wetu. ” Amesisitiza
Kauli hiyo ya Kinana imekuja kutokana hoja mbalimbali  ambazo zinaendelea kutolewa kuhusiana na suala la uwekezaji  wa kampuni ya DP World

Habari Zifananazo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button