Salif Keita ashindwa kutumbuiza Sauti za Busara

MWANAMUZIKI Mkongwe Salif Keita ameshindwa kufika Zanzibar na kutumbuiza katika Tamasha la Sauti za Busara 2026 kutokana na kuugua. Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Mkurugenzi wa tamasha hilo, Journey Ramadhani, amesema taarifa hiyo waliipokea kutoka kwa msanii huyo baada ya kushauriwa na daktari wake kutosafiri kwa sababu ya hali yake ya afya.

Journey amesema awali Salif Keita alikuwa tayari kuja pamoja na bendi yake na kutumbuiza siku ya mwisho wa tamasha, lakini daktari wake alimshauri asisafiri ili kulinda afya yake. SOMA: Tamasha Sauti za Busara kufanyika Mnazi Mmoja Hata hivyo, amesema kutokuwepo kwa Salif Keita hakutaathiri ubora wa tamasha hilo kwani bendi yake ilifika na kutumbuiza nyimbo zake maarufu kwa ustadi mkubwa.

Baada ya kumaliza onesho lao kwa wimbo wa Africa majira ya saa 7 usiku, wanamuziki hao hawakuzungumza na waandishi wa habari bali walielekea moja kwa moja Uwanja wa Ndege wa Abeid Amani Karume na kurejea nchini Mali.

 

Habari Zifananazo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button