Salma Kikwete aongoza kwa kishindo

DODOMA: KATIBU wa Itikadi na Uenezi wa CCM, CPA Amos Makala, ametangaza kuwa Salma Rashid Kikwete ameteuliwa kugombea ubunge Jimbo la Mchinga baada ya kuwa mgombea pekee aliyechukua na kurejesha fomu na kupitishwa.

” Salma  Rashid  Kikwete  alikuwa mgombea  pekee  aliyechukua fomu Jimbo la Mchinga  na amepitishwa  akiwa  mgombea  pekee ,” alisema  CPA  Amos  Makala. SOMA : Majina ya walioteuliwa CCM yanatangazwa

Katika majimbo mengine, Anna Killango Malecela ameongoza kura za maoni Jimbo la Same Mashariki, Hamida Mohammed Abdallah ameibuka kinara Jimbo la Lindi, huku Profesa Joyce Ndalichako akiongoza Jimbo la Kasulu Mjini.

 

Habari Zifananazo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button