RAIS Samia Suluhu Hassan, ameeleza kuridhishwa na utendaji kazi wa Waziri wa Madini, Dk Doto Biteko.
Rais Samia amempongeza Dk Biteko leo Oktoba 16, 2022, wakati akiwasalimu wananchi wa Runzewe, Jimbo la Bukombe, mkoani Geita na kuzungumza nao masuala mbalimbali akiwa safarini kuelekea mkoani Kigoma.
“Ndio maana mnaona nawagusa wote nawabadilisha, lakini Biteko yupo hapo katika Wizara ya Madini, kwa sababu ninaye kijana anayefanya kazi nzuri na anaisaidia Tanzania,” amesema Rais Samia.

Amesema mhango wa sekta ya madini katika pato la Taifa umeongezeka kutoka asilimia 4 na sasa unachangia karibu asilimia 8.
Amemtaka kuhakikisha mchango wa sekta ya madini unafikia asilimia 10, ifikapo mwaka 2025, ili iweze kuchangia zaidi katika pato la Taifa.