Samia ataka mashindano ya Kurani yaimarishe amani

RAIS Samia Suluhu Hassan ametaka mashindano ya kimataifa ya Kurani yatumike kudumisha amani, upendo na mshikamano.

Alisema hayo kwenye kilele cha mashindano hayo yaliyofanyika katika Uwanja wa Benjamini Mkapa, Dar es Salaam jana na kushirikisha wasomaji kutoka nchi mbalimbali duniani.

“Nimevutiwa na kaulimbinu ya mashindano haya, Kurani ni Amani. Kwa hiyo tumuombe Mungu Kurani itakayosomwa hapa na watoto na wakubwa kutoka mataifa mbalimbali, iwe dawa yetu Tanzania, vidumishe amani na mshikamano miongoni mwetu,” alisema Rais Samia.

Advertisement

“Nimepita hapa kusalimia kwa sababu naanza leo (jana) ziara mkoani Tanga. Nimefikiria kwa vile ugeni huu wa mashindano ni mkubwa na ni mara ya kwanza kuja nchini, ni vyema nikapitia kuwasalimu,” alisema.

Akizungumza katika mashindano hayo, Mufti wa Tanzania, Abubakar Zuberi aliungana na Rais Samia kuwasisitiza Watanzania kuipenda nchi yao kwa kudumisha amani.

“Niwaombe sana Watanzania, kuipenda nchi ni kudumisha amani, asiwepo wa kutokea au kujaribu kufanya ishara yoyote itakayoleta mmomonyoko na uharibifu wa amani,” alisema Mufti Zuberi.

Add a comment

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *