Samia ataka nidhamu kidato cha 4

RAIS Samia Suluhu Hassan amewatakia heri wanafunzi 595,816 wa kidato cha nne waliotarajiwa kuanza mtihani wa kuhitimu elimu ya sekondari katika shule za sekondari 5,868 nchini Novemba 17, 2025.

Kupitia ukurasa wake katika mtandao wa kijamii wa X, Rais Samia ameeleza kwamba idadi hiyo ya shule inatokana na nyongeza ya shule 305 ambazo ni mara yake ya kwanza kufanya mtihani wa kidato cha nne.

“Shule hizi ni matokeo ya kazi tunayoendelea kufanya kuhakikisha kila mtoto wa Tanzania ana uhakika wa kupata elimu bora. Mwenyezi Mungu Mtukufu aliyewaongoza tangu elimu ya awali hadi leo, awajalie utulivu muifanye na kukamilisha vyema hatua hii muhimu kwenye maisha yenu,” alieleza.

Aliongeza: “Nawaombea pia muendelee kuwa na nidhamu, upendo na bidii katika hatua zinazofuata kwenye maisha yenu. Serikali itaendelea kufanya kila inachoweza kuhakikisha ndoto zenu njema zinapata fursa na nafasi ya kukua na kustawi kwa manufaa yetu sote”.

SOMA: Watahiniwa 557,731 kufanya mtihani kidato cha nne

Wakati akizindua Bunge la 13, jijini Dodoma Novemba 14, Rais Samia alisema katika miaka mitano ijayo, pamoja na ajira za walimu, pia serikali itawekeza zaidi kwenye miundombinu ya shule mpya za awali, msingi na sekondari mpya na kuongeza madarasa kwenye shule zilizopo.

“Tutaendelea kuweka mkazo zaidi kwenye masomo ya Sayansi na Hisabati (STEM). Azma yetu ni kuongeza wanasayansi wabobezi katika eneo la sayansi ya data, akili unde, sayansi ya kompyuta na teknolojia za viwanda,” alisema.

Novemba 16, Baraza la Mitihani la Tanzania (NECTA) lilisema idadi ya watahiniwa wa kidato cha nne mwaka huu imeongezeka kwa asilimia 7.67 ikilinganishwa na mwaka jana.

Katibu Mtendaji wa Necta, Profesa Said Mohamed aliwaeleza waandishi wa habari Dar es Salaam kwamba watahiniwa 569,914 ni wa shule na 25,902 ni wa kujitegemea.

Profesa Mohamed alisema mitihani hiyo ingeanza Novemba 17 hadi Desemba 5, mwaka huu katika shule za sekondari 5,868 na vituo 813.

“Watahiniwa hawa 595,816 waliosajiliwa mwaka huu, wavulana ni 266,028 sawa na asilimia 46.68, huku  wasichana wakiwa 303,886 sawa na asilimia 53.32,” alisema.

Aliongeza, “Aidha, watahiniwa wa shule wenye mahitaji maalumu ni 1,128, wakiwemo 860 wenye uoni hafifu, 70 wasioona, 58 wenye uziwi, watano wenye ulemavu wa akili na 135 wenye ulemavu wa viungo.” Profesa Mohamed alisema.

Kwa watahiniwa wa kujitegemea, wavulana ni 10,862 sawa na asilimia 41.93 na wasichana 15,040 sawa na asilimia 58.07.

Necta imeagiza watahiniwa wafanye mtihani kwa kuzingatia kanuni za mitihani na kuepuka udanganyifu. Profesa Mohamed ameonya kwamba yeyote atakayebainika atafutiwa matokeo.

Habari Zifananazo

2 Comments

  1. I get paid over (90$ to 500$ / hour ) working from home with 2 kids at home. I never thought I would be able to do it but my best friend earns over $22000 a month doing this and she convinced me to try. it was all true and has totally changed my life… This is what I do, check it out by Visiting Following web….
    .
    HERE——————————————⊃⫸ http://Www.Cash43.Com

  2. Google is now paying $300 to $500 per hour for doing work online work from home. Last paycheck of me said that $20537 from this easy and simple job. Its amazing and earns are awesome. No boss, full time freedom and earnings are in front of you. This job is just awesome. Every person can makes income online with google easily……….
    .
    M­­­­­­o­­­­­­r­­­­­­e­ D­­­­­­e­­­­­­t­­­­­­a­­­­­­i­­­­­­l­­­­­­s For Us→→→→→→→→→→ http://Www.Payathome9.Com

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button