DAR ES SALAAM :Baraza la Mitihani (NECTA) limesema jumla ya watahiniwa 557,731 wamesajiliwa kufanya mtihani wa kidato cha nne 2024 kati yao watahiniwa wa shule 529,321 na watahiniwa wa kujitegemea ni 28,410
Watahiniwa 557,731 kufanya mtihani kidato cha nne
Mitihani hiyo itaanza kuanzia Novemba 11 hadi 29 mwaka huu hayo ameyasema na Katibu Mtendaji wa Baraza hilo, Dk.Said Mohamed kwenye mkutano na waandishi wa habari jijini Dar es salaam
“Jumla ya watahiniwa 557,731 wamesajiliwa kufanya mtihani wa kidato cha Nne 2024 ambapo kati yao watahiniwa wa Shule ni 529,321 na watahiniwa wa kujitegemea ni 28,410.”
“Kati ya watahiniwa wa Shule 529,321 waliosajiliwa mwaka 2024, wavulana ni 250,562 sawa na asilimia 47.34 na wasichana ni 278,759 sawa na asilimia 52.66. Aidha, wapo watahiniwa wa shule 1,088 wenye mahitaji maalum kati yao, wenye uoni hafifu ni 601, wasioona ni 56, wenye uziwi ni 209, wenye ulemavu wa akili ni 39 na wenye ulemavu wa viungo ni 183,”amesema Dk. Mohamed