Samia atengua uteuzi Mkurugenzi DART na kuteua

RAIS Samia Suluhu Hassan ametengua uteuzi wa Mkurugenzi Mtendaji wa Wakala wa Mabasi Yaendayo Haraka  (DART) Dk Edwin Mhede na nafasi yake kuchukuliwa na Dk Athuman Kihamia.

Taarifa ya Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais Ikulu, Zuhura Yunus inasema Dk Mdete atapangiwa kazi nyingine.

Dk Kihamia amewahi kuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Arusha.

Utenguzi wa Dk Mhede umekuja kufuatia malalamiko mengi kutoka kwa wananchi ikiwemo kusubiri mabasi kwa muda mrefu vituoni na kusababisha kero ya mlundikano wa abiria.

Kero nyingine inayolalamikiwa ni lugha chafu za wakatisha tiketi na kero nyingine nyingi.

Aidha, Rais Samia amemthibitisha Musa Kuji kuwa Kamishna wa Uhifadhi wa Shirika la Hifadhi za Taifa Tanzania (TANAPA).

Kuji alikua akikaimu nafasi hiyo.

Habari Zifananazo

Back to top button