Samia ateua, atengua apangia vituo mabalozi
RAIS Samia Suluhu Hassan amefanya uteuzi wa viongozi mbalimbali na kuwapangia vituo mabalozi.
Taarifa ya Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Dk Moses Kusiluka imewataja walioteuliwa ni pamoja na Rachel Kasanda anayekuwa Mkuu wa Wilaya ya Masasi akichukua nafasi ya John Kanoni ambaye uteuzi wake umetenguliwa.
Kwa mujibu wa taarifa hiyo iliyotolewa na Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, Ikulu, Sharifa Nyanga jana, Rais amemteua pia Ashraph Abdulkarim kuwa Meneja Mkuu wa Shirika la Masoko Kariakoo.
Mwingine aliyeteuliwa ni Profesa Jafari Kideghesho anayekuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini ya Mfuko wa Uhifadhi wa Wanyamapori Tanzania.
Kwa upande wa mabalozi waliopangiwa vituo ni Mobhare Matinyi aliyepangiwa kuwa balozi wa Tanzania nchini Sweden.
Mwingine ni Balozi Hamad Khamis Hamad aliyepangiwa kuwa Balozi wa Tanzania nchini Msumbiji.



