DODOMA: RAIS Samia Suluhu Hassan ametuma salamu za rambirambi kwa Kaimu Rais wa Namibia Dk Nangolo Mbumba, mke wa Rais, Monica Kalondo, na wananchi wake kufuatia kifo cha Rais wa taifa hilo, Hage Geingob.
“Kwa niaba ya wananchi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, natuma salamu za rambirambi kwa wananchi wa Jamhuri ya Namibia, Kaimu Rais, Mheshimiwa Dk Nangolo Mbumba, Mke wa Rais, Mheshimiwa Monica Kalondo, familia, marafiki na wandugu. katika SWAPO”
“Nimesikitika sana kupata taarifa ya kifo cha Rais wa Namibia, Mheshimiwa Hage Geingo ,ndugu mpendwa, mheshimiwa, Pan Africanist na rafiki mkubwa wa Tanzania.” Ameandika Rais Samia.
Rais wa Namibia, Hage Geingob (82) amefariki usiku wa kuamkia leo, wakati akipatiwa matibabu katika hospitali ya Lady Pohamba jijini Windhoek.
Geingob amekuwa Rais wa Namibia tangu mwaka 2015.