Samia awatakia Waislamu, Watanzania wote kheri ya Eid

RAIS Samia Suluhu Hassan amewatakia Waislamu na Watanzania wote kheri ya Sikukuu ya Eid al-Adha.
Kupitia kurasa zake rasmi za Instagram, Facebook na X, Rais Samia ameandika: “Tafakari na mafundisho ya Sikukuu hii yanatuasa kuishi katika utii kwa Mola wetu, katika ukweli na kumtegemea Mwenyezi Mungu, huku tukiwajali wenye uhitaji na wote ambao Mola amewaweka katika njia ya kuhudumiwa nasi kwa namna mbalimbali.
Sikukuu hii iendelee kutudumisha sote na Taifa letu katika amani, upendo na umoja. Mwenyezi Mungu Mtukufu aendelee kuzipokea na kuzikubali dua zetu katika yote mema kwa nchi yetu.
Eid al-Adha Mubarak.”