Samia: Chagueni Viongozi watakaotatua changamoto zenu
SINGIDA: KATIKA kuelekea uchaguzi wa Serikali za mitaa mwakani, Rais Samia Suluhu Hassan amewataka Wananchi kuhakikisha wanachagua viongozi sahihi watakaowatumikia katika kutatua chagamoto zao.
Akiwa ziarani katika Wilaya ya Mkalama, Mkoa wa Singida leo Oktoba 16, 2023 Rais Samia pia amewasihi washiriki wa nafasi mbalimbali za uongozi kuacha kuhubiri chuki na kugawa Wananchi wanaposhindwa katika chaguzi.
“Nawasihi kujitahidi sana kuepusha makundi, kwakuwa uchaguzi una mkono wa Mungu, ukikosa usilete chuki na kupelekea makundi ya kuwagawa watu,’ amesema Rais Samia.