Samia: Kheri ya Sikukuu ya Eid al-Fitr
RAIS Samia Suluhu Hassan amewataka Watanzania wote kuendelee kudumisha haki, umoja ,amani na mshikamano kwenye Sikukuu ya Eid al -Fitr.
Kupitia kurasa rasmi za mitandao za mkuu huyo wa nchi leo Aprili 10 amechapisha…
“Nawatakia Watanzania wote kheri ya Sikukuu ya Eid al-Fitr, tukimshukuru Mwenyezi Mungu mwingi wa rehema kwa baraka ya kuhitimisha funga na ibada ya Mwezi Mtukufu wa Ramadhani.
Mwenyezi Mungu atuonaye tunaposimama na mageuko yetu kati ya wanaosujudu, Mwenye kusikia na kupokea dua zetu; aendelee kutubariki na kudumisha Taifa letu katika haki, umoja, amani na mshikamano; katika misingi ya kufanya yaliyo mema, kujali na kutumikia wengine kwa upendo na weledi, na mioyo iliyojaa shukrani na ibada kwake” amechapisha Rais Samia