Samia kuanza ziara Tanga leo

Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Dk Batilda Burian amesema, Rais Samia ataanza ziara katika eneo la Mkata wilayani Handeni. Dk Burian aliwaeleza waandishi wa habari kuwa, Rais Samia atatembelea miradi ya maendeleo na pia, atazungumza na wananchi.

“Tunapaswa kuonesha mshikamano wetu kwa kujitokeza kwa wingi siku ya mapokezi yake. Serikali yake imefanya kazi kubwa ya maendeleo na ni fursa yetu kuthibitisha uung waji mkono wetu kwake,” alisema.

Dk Burian alisema, Rais Samia atazindua mradi wa uboreshaji wa Bandari ya Tanga, Hospitali ya Wilaya ya Handeni na Jengo la ofisi ya Halmashauri ya Mji wa Handeni. Alisema pia, atajionea maendeleo ya ujenzi wa daraja la Mto Pan gani, atafungua shule ya sekondari ya wasichana ya mkoa, atatembelea mradi wa umwagiliaji na mradi wa miji 28 unaotekelezwa katika wilaya nne za Mkoa wa Tanga.

“Rais akiwa mkoani hapa atapata fursa ya kufanya mikutano ya hadhara pamoja na kuzungumza na makundi mbalimbali ya watu waki wemo wazee”.

Habari Zifananazo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button