Samia mgeni rasmi siku ya wanawake duniani

DAR ES SALAAM: RAIS Samia Suluhu Hassan anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika kilele cha Maashimisho ya Siku ya Wanawake Duniani yatakayofanyika kitaifa mkoani Arusha Machi 8, mwaka huu.

Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia , Wanawake na Makundi Maalumu, Dk Doroth Gwajima amesema hayo Dar es salaam wakati akizungumza na waandishi wa habari. Aidha kauli mbiu ni‘ Wanawake na Wasichana Tuimarishe Usawa, Haki na Uwezeshaji’.

Awali, Dk Doroth alisema kuwa maadhimisho hayo hufanyika kila mwaka katika ngazi za mikoa lakini hufanyika kitaifa kila baada ya miaka mitano lengo ikiwa ni kupima na kutathmini utekelezaji wa malengo na makadorio haliyowekwa katika kufikia usawa wa kijinsia na uwezeshaji wa wanawake nchini.

“Kwahiyo ningependa kutaarifu umma wa watanzania, wadau, taasisi pamoja na sekta binafsi kuwa mwaka 2025 maadhimisho haya ya siku ya wanawake duniani yatafanyika katika mkoa wa Arusha na yataendelea kuadhimishwa katika ngazi ya mikoa nchi nzima ili kuwa na ushiriki wa wanawake na watu wote,” alisema Dk Doroth.

Aliongeza kuwa sababu mahususi ya Arusha ya kupewa heshima ya kufanyika kwa maadhimisho hayo ni kuwa haukjawahi kufanyika maadhimisho ya aina hiyo katika kanda hiyo na mikoa ya Arusha na Manyara inaongoza kwa changamoto kubwa za wanawake zikiwemo masuala ya ukeketaji.

Aidha, Dr Doroth alisema kuwa katika masuala ya ukeketaji mikoa hiyo inaongoza kwa asilimia 43 ikifuatiwa na mkoa wa Mara wenye asilimia 28 ukilinganisha na mikoa mingine ambayo takwimu zake zimepungua, hivyo kwa kufanya hivyo jamii itaweza kuona ili kuweza kutatua changamoto hizo.

Katika hatua nyingine alisema maadhimisho hayo yamebeba sura ya kipekee kwani yameambatana na miaka 30 ya utekelezaji ya azimio la ulingo la Beijing lililofanyika 1995 la wanawake waliokaa kikao na kufikia maazimio mbalimbali na Tanzania ikiwa ni moja ya mwanachama wa jumuiya ya Umoja wa Mataifa(UN) imeendelea kutekeleza maazimio hayo.

Dk Doroth alisema kuwa serikali imeunds kamati ya kitaifa ya maandalizi na kufafanua baadhi ya matukio yatakayokuwa yakifanyika kuelekea maadhimisho hayo ya siku ya wanawake.

Alisema kuwa Machi mosi, mwaka huu uzinduzi utafanyika katika ngazi za mikoa, wilaya na kata kwa kushirikisha wanawake na wadau wote katika maeneo , uzinduzi huo utaambatana na jamii kutathmini utekelezaji wa maazimio ya Beijing na kuweka muelekeo wa utekelezaji katika maeneo hayo.

Machi 3 hadi 6 yatafanyika makongamano ya kikanda katika kanda saba na mikoa itakayohusika ni Dar es salaam, Arusha, Dodoma, Geita, Mbeya, Lindi na Kigoma na kila mkoa utakuwa na ajenda zao ambazo zitatangazwa kwa ajili ya kujadiliwa kwenye makongamano hayo.

Machi 5 hadi 8 alisema kutakuwa na maonyesho ya wanawake, taasisi za umma na binafsi na kampuni mbalimbali yatakayofanyika mkoani Arusha na Machi saba kumeandaliwa usiku maalumu wa mwanamke ambao unatarajiwa kuhudhuriwa na watu takribani 1,500 mkoani Arusha.

Aliongeza kuwa Machi 8 ndio kilele cha maadhimisho hayo na kwa kutambua umuhimu wa siku hiyo kutakuwa na sare maalumu kwa taifa zima ya kitenge ambacho kitapatikana kwa Sh 25,000 kwa bei ya jumla na haitozidi Sh 30,000 kwa bei ya rejareja vyenye rangi mbalimbali ambavyo kwa pamoja vinachora rangi ya bendera ya taifa.

Sambamba na hayo alitoa historia fupi ya maadhimisho hayo alisema 1977 umoja wa matifa uliweka azimio linalozitaka nchi mwanachama wa umoja huo kuadhimisha siku ya wanawake kila ifikapo Machi 8 kila mwaka ikiwa ni kuenzi mchango wa wanawake katika ujenzi wa taifa.

Alisema chimbuko la siku ya wanawake duniani ni jitihada za wanawake wafabyakazi wa sekta ya viwanda nchini marekani ambao 1911 walifanya maandamano ya kupinga mazingira duni ya kazi na kuwepo kwa unyanyasaji katika ajiwa ikiwa ni kulipwa mshahara mdogo kwa kazi iliyosawa na ile ya wanaume.

Tanzania ilianza kuadhimisha siku ya wanawake duniani 1997 na kujiwekea utaratibu wa kufanyika kila mwaka katika ngazi za mikoa na kuadhimisha kitaifa kila baada ya miaka mitano.

Habari Zifananazo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button