ZURICH : MASHIRIKA mawili ya kutetea haki za binadamu duniani Amnesty na Right Alliance(SRA), wameliomba Shirikisho la Soka Duniani -FIFA kusitisha mchakato wa kuichagua Saudi Arabia kuwa mwenyeji wa michuano ya soka ya Kombe la Dunia mwaka 2034.
Mashirika hayo yamedai kuwa FIFA haina sababu ya kupiga kura kuichagua Saudi Arabia kuwa mwenyeji wa michuano hiyo hadi hapo itakapokubaliana kutekeleza mikataba mbalimbali ya kutetea haki za binadamu na kufanya mageuzi makubwa ya mikakati hiyo..
Tathmini iliyofanywa na mashirika haya imebaini kuwa hakuna pendekezo lolote lililoainisha la kufikia viwango vya haki za binaadamu vinavyotakiwa viwepo ndani ya shirikisho hilo.
Wamesema michuano hiyo kufanyika nchini Saudi Arabia itakabiliwa na ukiukwaji mkubwa wa haki za binadamu. SOMA: Saudi Arabia kuandaa kombe la dunia 2034