UFARANSA: Saudi Arabia imeshawasilisha stakabadhi zake za kuonyesha nia ya kugombea kuandaa Kombe la Dunia la 2034 katika mji mkuu wa Ufaransa.
Stakabadhi hizo zilikabidhiwa na Mwanamfalme Abdulaziz bin Turki bin Faisal, Waziri wa Michezo, Mwenyekiti wa Kamati ya Olimpiki na Walemavu ya Saudia, na Rais wa Shirikisho la Soka la Saudia, Yasser Al-Meshal, pamoja na watoto wawili kutoka vituo vya mafunzo vya kikanda vya Chama cha Soka cha Saudi Arabia.
“Ufalme una nia ya kuandaa tukio muhimu zaidi katika ulimwengu wa soka, na hivyo kuthibitisha nafasi yake kubwa, yenye ushawishi na chanya kwenye ramani ya dunia nzima, katika nyanja mbalimbali, ikiwa ni pamoja na michezo.”amesema Waziri wa michezo wa Saudia