USWISI : SAUDI ARABIA imepoteza kiti cha ujumbe kwenye Baraza la Haki za Binadamu la Umoja wa Mataifa kufuatia kampeni ya makundi ya haki za binaadamu yanayolilaumu taifa hilo kukiuka haki za binadamu.
Baraza hilo ambalo linawanachama 193 hapo jana liliwachaguwa wajumbe wapya 18 kuingia kwenye Baraza la Haki za Binaadamu lenye wajumbe 47, ambao hupatikana kwa mujibu wa maeneo ili kuhakikisha uwakilishi wa kijiografia.
Kabla ya zoezi la kupiga kura, mkurugenzi wa shirika la Human Rights Watch, Louis Charbonneau, aliitaja Saudi Arabia haina sifa kuingia katika Baraza la Haki za Binaadamu.
Baraza hilo lililoundwa mwaka 2006 na lenye makao yake makuu mjini Geneva, Uswisi, huwa linafanya tathmini za haki za binaadamu kwa nchi zote kila baada ya muda na kutoa ripoti kamili zinazohusu haki za binadamu ambapo Saudia Arabia imebainika haina sifa ya kushiriki katika baraza hilo.
Nchi ambazo zilizoingia kwenye Baraza hilo kutoka eneo la Asia na Pasifiki mwaka huu ni Thailand, Cyprus, Qatar, Korea Kusini na Visiwa vya Marshall.
SOMA : Mambo mazuri ushirikiano Tanzania, Saudi Arabia
==