Sekta binafsi zaitwa uzalishaji mbegu kanda ya ziwa

KARAGWE: Taasisi ya Udhibiti wa Ubora wa Mbegu Tanzania (TOSCI) imezitaka sekta binafsi kuwekeza zaidi katika uzalishaji wa mbegu kwenye mikoa ya Kanda ya Ziwa kutokana na hali ya hewa yenye vigezo vinavyokidhi kuzalisha mbegu bora.

Mkurugenzi Mkuu wa TOSCI, Dk Nyasebwa Chimagu ametoa wito huo leo Mei 12, 2026 alipotembelea shamba la uzalishaji wa mbegu la Kahama Fresh lililopo wilayani Karagwe mkoani Kagera.

Akiwa eneo hilo, Dk Chimagu amesema sekta binafsi zinapaswa kuwekeza zaidi katika uzalishaji wa mbegu katika mikoa hiyo, hususan Mkoa wa Kagera wenye maeneo makubwa ya kilimo, jambo litakalosaidia kupunguza gharama za uzalishaji.

Katika ziara yake amevutiwa na uwekezaji wa uzalishaji wa mbegu za mahindi katika shamba mwenkezaji wa Kahama Fresh na kudai kuwa atakuwa mdau mkubwa wa kuongeza na wawekezaji wa mbegu Kuja kuwekeza kwani soko ni la uhakika.

Amesema uwezo wa nchi kuzalisha mbegu kwa sasa ni tani 79,000 wakati mahitaji halisi ni tani 127,000 ambapo Tanzania sasa inazalisha asilimia 80 na uwekezaji wa wadau utapunguza athari za kuagiza mbegu nje ya nchi

Meneja msaidizi wa Kampuni Fresh, Oswald Sylivester amesema kwa sasa mbegu zimepandwa katika hekta 500 na mwanzoni ilikuwa ni kupanda na hekta 800.

Amesema changamoto kubwa inayowakabili ni mabadiliko ya hali ya hewa ambapo wamelazimika kutengeneza mabwawa madogo ya umwagiliaji ili kuzalisha mbegu bora za mahindi katika hekta 1,000.

Habari Zifananazo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button