Sekta ya afya yatikiswa na pengo la misaada

LONDON : UTAFITI mpya uliotolewa na jarida la Lancet umebainisha kuwa usitishaji mkubwa wa misaada ya kimataifa utapunguza kwa kiasi kikubwa ufadhili wa miradi ya afya duniani.

Kwa mujibu wa utafiti huo, ufadhili huo unatarajiwa kushuka kutoka dola bilioni 80 mwaka 2021 hadi dola bilioni 39 mwaka huu ikiwa ni kiwango cha chini zaidi ndani ya miaka 15.

Takwimu hizo zinaashiria athari kubwa kwa sekta ya afya kimataifa, hasa kwa mataifa yenye utegemezi mkubwa wa misaada kama Somalia, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo na Malawi.

Mataifa hayo yanakabiliwa na hatari ya kupoteza huduma muhimu za afya kwa mamilioni ya raia wao. SOMA: Trump apunguza misaada, watoto waathirika

Hatua hiyo ya kupunguza misaada, iliyochukuliwa na mataifa tajiri kama Marekani, Uingereza, Ufaransa na Ujerumani, imeelezwa na watafiti kuwa italazimisha dunia kuchukua hatua kali za kubana matumizi katika huduma za afya, jambo ambalo linaweza kuongeza hatari ya milipuko ya magonjwa na vifo vinavyoweza kuzuilika.

 

Habari Zifananazo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button