Trump apunguza misaada, watoto waathirika

MADRID , UHISPANIA : TAKRIBAN watu milioni 14 wanaoishi katika mazingira magumu duniani wako hatarini kufariki dunia kufikia mwaka 2030, kufuatia hatua ya Rais wa Marekani, Donald Trump, kupunguza misaada ya kibinadamu.

Kwa mujibu wa utafiti mpya uliotolewa leo na Jarida la tiba la The Lancet, theluthi moja ya watu hao ni watoto wadogo, ambao maisha yao yanategemea kwa kiasi kikubwa msaada wa kimataifa. SOMA: Maambukizi ya Ukimwi kuongezeka mara sita 2029

Watafiti wa kimataifa wameeleza kuwa kati ya mwaka 2001 hadi 2021, ufadhili wa Shirika la Maendeleo la Kimataifa la Marekani (USAID) uliokoa maisha ya watu wapatao milioni 91 katika nchi zinazoendelea. Hata hivyo, kupungua kwa ufadhili huo kunaweza kupelekea vifo zaidi ya milioni 14 vinavyoweza kuzuilika.

Ripoti hiyo imechapishwa wakati viongozi wa dunia na wafanyabiashara wakikutana kwenye mkutano wa Umoja wa Mataifa nchini Uhispania, wakijadili njia za kuimarisha sekta ya misaada ya kibinadamu ambayo inakumbwa na changamoto kubwa.

Kabla ya Trump kurejea Ikulu mwezi Januari, USAID ilikuwa ikichangia zaidi ya asilimia 40 ya msaada wa kibinadamu duniani kote. Hatua ya kupunguza ufadhili imeibua wasiwasi mkubwa kuhusu mustakabali wa huduma za afya, lishe, na maji safi kwa jamii zilizo hatarini.

Habari Zifananazo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button