Sekta ya fedha yatakiwa kusukuma nishati safi ya kupikia

SERIKALI imezitaka taasisi kutoka sekta ya fedha nchini kuanzisha huduma na bidhaa za kifedha zitakazosaidia kusambaza matumizi ya nishati safi ya kupikia, hususan kwa wajasiriamali wadogo, maeneo ya pembezoni na vijijini pamoja na wabunifu wa teknolojia.
Wito huo umetolewa jana Februari 4, 2026 na Naibu Waziri wa Nishati, Salome Makamba, alipomwakilisha Waziri wa Nishati katika uzinduzi wa mradi wa nishati safi ya kupikia katika Shule ya Sekondari Bunge Wasichana mkoani Dodoma. SOMA: Serikali kuwaunga mkono wadau nishati safi
Makamba amesema Tanzania imepiga hatua katika matumizi ya nishati safi ya kupikia kutoka asilimia 6.9 mwaka 2021 hadi asilimia 23.2 mwaka 2025, lakini bado takribani asilimia 77 ya kaya zinatumia nishati isiyo safi. “Hii inahitaji ushirikiano wa karibu kati ya Serikali na sekta binafsi ili kuhakikisha nishati safi ya kupikia inawafikia wananchi wengi zaidi, hususan vijijini,” alisema.
Pia amewataka wasambazaji wa gesi za mitungi kuongeza vituo vya usambazaji na ujazaji, huku wabunifu na vijana vyuoni wakihamasishwa kufanya tafiti na kubuni teknolojia rafiki kwa mazingira. Kuhusu mradi huo, Makamba alisema ni utekelezaji wa agizo la Serikali kwa taasisi zinazohudumia watu zaidi ya 100 kutumia nishati safi ya kupikia ili kulinda afya na mazingira.

Ameongeza kuwa mfumo huo unaharakisha upishi, hupunguza gharama na kuondoa madhara ya moshi kwa wapishi na wanafunzi. Makamba alisema juhudi hizo ni sehemu ya mkakati wa kitaifa unaoongozwa na Rais Samia Suluhu Hassan wa kuhakikisha asilimia 80 ya Watanzania wanatumia nishati safi ya kupikia ifikapo mwaka 2034.
Katika shule hiyo, alizindua pia Klabu ya Nishati Safi ya Kupikia (Clean Cooking School Club), ya kwanza nchini, itakayotoa elimu na kuhamasisha matumizi ya nishati safi mashuleni na katika jamii.
Awali, Mkuu wa Shule ya Sekondari Bunge Wasichana, Richard Msana, amesema shule hiyo imepunguza kwa kiasi kikubwa gharama za nishati baada ya kuacha kutumia kuni na kuhamia gesi, hali iliyopunguza matumizi kutoka zaidi ya Sh milioni 10 kwa miezi mitatu hadi wastani wa Sh milioni 1.3 kwa mwezi.




https://youtube.com/shorts/db-a_3qIlNs?si=7pkEvVyvx044_n3X
I just came across this amazing way to earn $6,000-$8,000 a week online! No selling, no struggle—just a simple system that anyone can follow. Mia Westbrook did it, and so can you! Don’t miss out on this life-changing opportunity.
.
Follow Here ……………………… https://Www.Cash54.Com
I am making a real GOOD MONEY (300$ to 400$ / hr )online from my laptop. Last month I GOT check of nearly 18,000$, this online work is simple and straightforward, don’t have to go OFFICE, Its home online job. At that point this work opportunity is for you.if you interested.simply give it a shot on the accompanying site….Simply go to the BELOW SITE and start your work…
.
More Details For Us→→→→→→→→→ https://Www.Payathome9.Com
https://youtube.com/shorts/db-a_3qIlNs?si=7pkEvVyvx044_n3X
https://youtube.com/shorts/db-a_3qIlNs?si=7pkEvVyvx044_n3X
https://youtube.com/shorts/db-a_3qIlNs?si=7pkEvVyvx044_n3X
https://youtube.com/shorts/db-a_3qIlNs?si=7pkEvVyvx044_n3X