Sekta ya madini yaongoza fedha za kigeni

RAIS Samia Suluhu Hassana amesema Sekta ya Madini ndiyo inayoongoza kwa kuliingizia taifa fedha nyingi za kigeni.

Akizungumza wakati wa kufunga Maonesho ya Saba ya Teknolojia na Uwekezaji kwenye Sekta ya Madini mkoani Geita, kiongozi huyo wa nchi amesema mwaka 2023, sekta hiyo iliingiza takriban asilimia 56 ya fedha zote za kigeni.

Advertisement

“Sekta hii iliingiza takriban asilimia 56 ya fedha zote za kigeni zilizoingia nchini,” amesema Rais Samia.

Rais Samia amesema serikali inatoa uzito mkubwa kwenye sekta hiyo kwa kutambua nafasi yake katika kubadili hali za wananchi hususan wachimbaji wadogo.