‘Sekta ya usafirishaji inahitaji wataalamu wa kutosha’

WAZIRI wa Uchukuzi, Profesa Makame Mbarawa amesema sekta ya usafirishaji inahitaji wataalamu wa kutosha kwa ajili ya kufanya kazi katika miradi ya kimkakati inayoendelea nchini.
Pia amekipongeza Chuo cha Taifa cha Usafirishaji (NIT) kwa kuendelea kufanya tafiti zinazoboresha sekta hiyo.
Profesa Mbarawa ameyasema hayo leo Dar es Salaam, wakati akifungua mkutano wa kwanza wa Kimataifa wa usafirishaji na usambazaji ulioandaliwa na NIT.
Amesema serikali imewekeza kwenye miradi mbalimbali na kwamba uwekezaji huo unaendana na tafiti kutoka kwa wataalamu sambamba na kuwajengea uwezo watanzania kufanya kazi katika miradi hiyo.
‘’Tunaipongeza NIT kwa kuandaa mkutano huu, ukweli ni kwamba nchi yoyote duniani haiwezi kuendelea kama haina sekta mahiri ya usafirishaji kwa mfano, mizigo itakuja hapa Dar es Salaam lazima iwafikie Watanzania mbalimbali,’’ amesema Profesa Mbarawa.
Ameeleza kuwa: ‘’Tunahitaji wataalamu ambao wametayarishwa vizuri na sio waliopikwa nusunusu hivyo ninyi kama wataalamu mnapaswa kufanya kazi hiyo. Hii itatusaidia kupata nguvu kazi sahihi katika miradi inayoendelea,’’ amesema.
Profesa Mbarawa amesema kuendeleza miradi hiyo inahitaji wafanyakazi na wataalam na kwamba NIT kwa kushirikiana na wataalamu kutoka nje ya nchi, watayarishe wataalam wazuri ambao wataitoa nchi kutoka mahali ilipo na kukuza uchumi kwa wananchi wetu ambao kwa kiasi kikubwa wanategemea sekta ya usafirishaji.
Alifafanua kuwa wakati wanaendelea na ujenzi wa miundombinu, wataalamu watahitajika kwani miundombinu yote haiwezi kujiendesha yenyewe.
‘’Tumesaini mkataba wa Sh bilioni 630 kwa ajili ya kujenga karakana ya meli katika bandari ya Kigoma, kwa kujenga meli mbili kwa ajili ya kusafirisha mizigo na meli moja itakuwa na uwezo wa kubeba tani 3,500 ambayo itasafiri kupitia Ziwa Tanganyika na meli ya pili itasafiri Ziwa Victoria ikiwa na uwezo wa kubeba tani 3,000,’’ alisema.
Waziri huyo amesema ni mara ya kwanza katika historia kuwahi kujenga kiwanda kamili chenye vifaa vyote vya kisasa vinavyohusika na ujenzi wa meli na alitoa mfano wa kiwanda cha Afrika Marine cha Mombasa na Kampuni ya Secco kwamba wana viwanda hivyo lakini havina vifaa vya kisasa kwa sababu ni vya zamani.
”Tunaenda kuanzisha utaratibu wa door to door transport mfanyabiashara wa Congo akichukua biashara yake hapa anaingiza kwenye gari kutoka hapa hadi kigoma akifika kigoma anaingiza hiyo gari kwenye meli hadi Congo,” amefafanua.
Kwa upande wake, Mkuu wa Chuo cha NIT, Profesa Zacharia Mganilwa amesema kuwa taasisi za elimu ya juu zina majukumu matatu ikiwemo kufundisha, kufanya utafiti na kutoa ushauri wa kitaalamu hivyo kupitia mkutano huo, watafiti watatoa matokeo ya tafiti walizozifanya kwa kushirikiana na nchi zilizoendelea.
”Mkutano huu unakwenda kutoa majibu au takwimu zitakazowafanya wanaoendesha mashirika mbalimbali ya uchukuzi hapa nchini kama vile Shirika la Reli Tanzania (TRC), Wakala wa Mabasi yaendayo haraka (DART) na Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA), ambao wataifanya sekta yetu ya uchukuzi na usafirishaji iweze kufanya utendaji wenye tija kwa matumaini makubwa ya serikali ilivyowekeza na matumaini kwa wananchi waweze kupata huduma nzuri katika usafirishaji,”amesema.
Profesa Mganilwa ameeleza kuwa tafiti ndiyo zilizowasaidia kuanzisha programu mpya ikiwemo mitaala ya wataalamu wa reli kuanzia wahandisi hadi menejimenti ya mashirika ya reli.
My last salary was $8,750 only worked 12 hours a week. My longtime neighbor estimated $15,000 and works about 20 hours for seven days. I can’t believe how blunt vs04 he was when
I looked up his information,
For More Details…… http://Www.Smartcash1.com
★My buddy’s mother makes $90 per hour working on the computer (Personal Computer). ( e06q) She hasn’t had a job for a long, yet this month she earned $15,500 by working just on her computer for 9 hours every day.
Click and Copy Here══════►►► http://Www.SmartCareer1.com
I’ve gained only within four weeks by comfortably working part-time from home. Immediately when I had lost my last business, mtg I was very troubled and thankfully
following website___________ http://Www.Careers12.com