Sekta za fedha zapongezwa kuwawezesha wanawake kiuchumi

WAZIRI wa Viwanda na Biashara, Judith Kapinga, ameipongeza Benki ya  CRDB kwa mchango wake mkubwa katika kuwainua wajasiriamali nchini kupitia utoaji wa elimu ya fedha na fursa za mitaji, hatua inayosaidia kukuza uchumi jumuishi na endelevu.

Akizungumza katika hafla ya Kitchen Party Gala 2026 iliyofanyika jijini Dar-es-salaam, Waziri Kapinga amesema ushirikiano kati ya sekta ya fedha na wajasiriamali ni muhimu katika kupunguza umasikini na kuimarisha maendeleo ya kiuchumi, huku akisisitiza kuwa wanawake wana nafasi kubwa katika ustawi wa familia na taifa.SOMA: Mwongozo uwezeshaji wanawake wazinduliwa

Kwa upande wake, Benki ya CRDB  imeendelea kujikita katika kuwawezesha wajasiriamali wadogo na wachanga kupitia bidhaa na huduma za kifedha zinazolenga kuongeza ujuzi, mitaji na uwezo wa ushindani sokoni, sambamba na kusisitiza nidhamu ya matumizi ya fedha kwa maendeleo endelevu.

Habari Zifananazo

2 Comments

  1. l Get paid over $110💸 per hour working from home. l never thought I’d be able to do it but my buddy makes over $22174💸 a month doing this and she convinced me to try.Single Mom Reveals How She Earns 88k/Yr Working 10 Hrs/Week From Home The possibility with this is endless____ https://FindJobs1.Site

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button