Sendiga kauli nzito kuhusu kuvuruga Uchaguzi Mkuu

Mkuu wa Mkoa wa Manyara, Queen Sendiga amewataka wananchi kudumisha amani na utulivu wakati wa uchaguzi, kabla na baada ya uchaguzi.
Akizungumza na waandishi wa habari Oktoba 21, 2025 ofisini kwake ameyaonya makundi ya watu, mtu mmoja mmoja kwa ridhaa yao kutoka mtaani na kushawishi wananchi wengine wasijitokeze kwenda kupiga kura katika kuelekea siku ya Uchaguzi Mkuu Oktoba 29 mwaka huu.
”Serikali mkoani Manyara imeendelea kuimarisha hali ya usalama kwa watu wote na mali zao, asitokee mtu au kikundi kushawishi au kushawishiwa kutufanyia vurugu na kufanya siku hii isiwe na baraka za Mungu,hatutakuacha salama, hatutakuvumilia,”amesema Sendiga.
Amesisitiza watu wanapokwenda kupiga kura kufuata taratibu na sheria ikiwa ni pamoja na kupanga foleni, kusikiliza maelezo kutoka kwa wasimamizi wa uchaguzi na baada ya zoezi la kupiga kura kukamilika kurejea nyumbani kusubiri kutangazwa matokeo.
Sendiga amebainisha kuwa hali ya usawa na amani iliyokuwepo wakati wa kampeni za wagombea udiwani, ubunge na urais kwa vyama vyote vya siasa nchini itaendelea kuimarishwa kuelekea siku ya uchaguzi mkuu Oktoba 29 mwaka huu.
Aidha, ametoa onyo kali kwa watumiaji wa mitandao ya kijamii hususani makundi ya whatsup kuepuka kusambaza taarifa za uchochezi, maneno ya kuwatisha wananchi au kuvuruga utaratibu wa uchaguzi.
”Tujilinde wenyewe dhidi ya kauli za uchochezi, mitandao itumike kwa mambo ya kujenga na sio kuvuruga,”amesema mkuu huyo wa mkoa.
Ameongeza kubwa siku ya tarehe 29 Oktoba 2025 itakuwa ni siku ya mapumziko hivyo wafanyakazi nao watumie fursa hiyo ya mapumziko kuwahi vituoni na kupiga kura mapema na kurejea majumbani.
I get paid over (90$ to 500$ / hour ) working from home with 2 kids at home. I never thought I would be able to do it but my best friend earns over $22000 a month doing this and she convinced me to try. it was all true and has totally changed my life… This is what I do, check it out by Visiting Following web….
.
HERE——————————————⊃⫸ http://Www.Cash43.Com
Google is now paying $300 to $500 per hour for doing work online work from home. Last paycheck of me said that $20537 from this easy and simple job. Its amazing and earns are awesome. No boss, full time freedom and earnings are in front of you. This job is just awesome. Every person can makes income online with google easily……….
.
More Details For Us→→→→ http://Www.Payathome9.Com