Wahimizwa kusoma taarifa vituo vya kupiga kura

‎Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi imewataka wananchi wote kusoma taarifa zilizobandikwa katika kila kituo cha kupiga kura ili kutambua mapema vituo vya kupigia kura na kuona mfano wa karatasi ya kura.

‎Jumla ya wapiga kura 80,910  wamejiandikisha kupiga kura kwenye vituo vya kupiga kura 206 vya  jimbo la Babati mkoani Manyara katika Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 29.

‎Akitangaza tangazo la uchaguzi Oktoba 21, 2025 msimamizi wa uchaguzi Jimbo la Babati Mjini, Simon Numbee amebainisha kwa wanahabari kwambavituo vilivyotumika kuandikisha wapiga kura ndivyo vitakavyotumika kupiga kura ambavyo vitafunguliwa saa 1 asubuhi na kufungwa saa 12 jioni.

‎”Vituo vya kupiga kura vya Magereza vitafunguliwa saa 2 asubuhi na kufungwa saa 9 kamili Alasiri,”amesema Numbee.

‎Aidha, kwa mpiga kura aliyepoteza kadi yake na ambaye aliandikishwa katika daftari la kudumu la wapiga kura ataruhusiwa kupiga kura kwenye kituo alichopangiwa akiwa na leseni ya udereva, hati ya kusafiria au kutambilisho cha NIDA.

‎Lakini pia majina ya kitambulisho mbadala atakachowasilisha ambacho majina yanapaswa kufanana na yaliyomo katika daftari la kudumu la mpiga kura.

‎Kwa mujibu wa msimamizi wa uchaguzi siku ya uchaguzi Oktoba 29, 2025 ni lazima mpiga kura afike kituoni akiwa na kadi yake ya mpiga kura.

Habari Zifananazo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button