Sera mpya kudhibiti uagizwaji magari chakavu

WAZIRI wa Nchi, Ofisi ya Rais, Mipango na Uwekezaji, Profesa Kitila Mkumbo amesema serikali ipo katika mpango wa kutengeneza sera ya itakayodhibiti uingizwaji wa magari.

Profesa Mkumbo ametoa kauli hiyo jana wakati wa ziara yake ya kikazi ya kukagua hali ya uzalishaji katika kiwanda cha kuunganisha magari cha GF Vehicle Assemblers Limited kilichopo Kibaha mkoani Pwani.

Amesema kulingana na sera iliyopo kwa sasa inaruhusu mtu kuagiza gari chakavu hata kama lina miaka zaidi ya 50 na kwamba lengo ni kudhibiti hali hiyo.

“Magari yanayoingizwa nchini mengi yanakuwa mabovu ambapo ili viwanda vya magari vilivyopo nchini viweze kwenda mbali lazima yuje na sera ambayo itazuia uingizaji wa magari chakavu na watu watumie magari mapya yanayozalishwa nchini,”amesema.

Amesema uwekezaji wa kiwanda hicho kwa hatua ya awali ilikuwa na mtaji wa Sh bilioni 10 na sasa mtaji huo umekuwa zaidi kiasi ambacho kimepelekea kuzalisha magari mengi huku kikisaidia kutoa ajira kwa Watanzania 220.

Mkumbo amesema kuwa kwa niaba ya Watanzania kupitia Serikali ya Chama Cha Mapinduzi ( CCM ) chini ya Rais Samia Suluhu Hassan ina mipango mikubwa ya kuendelea kuhakikisha kwamba Tanzania inakuwa na Viwanda vyakudumu.

Kwa upande wake meneja mkuu wa kiwanda hicho, Ezra Mereng amesema kuwa kupitia kiwanda hicho ,vijana wakitanzania wanaweza kuunganisha magari kwa viwango vya kimataifa huku ndoto za kiwanda hicho ni kuunganisha magari makubwa na madogo.

Aidha, Mireng alimshukuru Waziri Mkumbo pamoja na timu yake kutoka kituo cha uwekezaji nchini Tanzania (TIC) kwa namna ambavyo wamesaidia kiwanda hicho kufikia mafanikio yaliyopo hivi sasa.

Kiwanda hicho kilichopo eneo la Tamco- Kibaha Mjini kinaunganisha magari makubwa ya mizigo aina ya FAW yenye uwezo wa kubeba mzigo tani 30.

Habari Zifananazo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button