Serengeti Boys ilivyotwaa ubingwa CECAFA U-17

ETHIOPIA; Picha za matukio mbalimbali wakati timu ya Taifa ya vijana ya Tanzania chini ya umri wa miaka 17 (Serengeti Boys) ilipotwaa ubingwa wa michuano ya Baraza la Mpira wa Miguu Afrika Mashariki na Kati (CECAFA) kwa kuifunga Uganda mabao 3-2 Uwanja wa Abebe Bikila nchini Ethiopia jana.

Licha ya kuwa bingwa, Serengeti Boys imefuzu kucheza fainali ya Mataifa ya Afrika (AFCON) 2026 kwa mara ya pili mfululizo pamoja na Uganda na Ethiopia ambao waliifunga Kenya kwa mabao 3-0 katika mchezo wa kutafuta mshindi wa tatu. (Picha kwa hisani ya TFF).



