Serikali haijengi shule kujifurahisha – Msonde

RUVUMA; NAIBU Katibu Mkuu Elimu, Ofisi ya Rais-TAMISEMI ,Dk Charles Msonde amesema Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Rais Samia Suluhu Hassan inajenga shule mpya nchini ili kutatua changamoto ya watoto kutembea umbali mrefu kufuata elimu na kuondoa msongamano wa wanafunzi darasani.

Dk Msonde amesema hayo katika ziara ya kukagua maendeleo ya ujenzi wa shule mpya ya Sekondari Mputa inayojengwa kupitia fedha za mradi wa SEQUIP Wilaya ya Namtumbo mkoani Ruvuma.

Amesema, serikali haijengi shule kwa sababu ya kujifurahisha au kumridhisha mtu bali inajenga shule kwa lengo la kuwawezesha watoto wasitembee umbali mrefu kufuata elimu.

“Lengo ni kuwawezesha watoto wa kitanzania wanaoingia sekondari kumaliza masomo bila kisingizio cha umbali ili waondoke na ujuzi na umahiri wa kujiletea maendeleo yao pamoja na kuleta maendeleo ya jamii zao na taifa kwa ujumla,” amesema.

Aidha, ameupongeza uongozi wa Halmashauri ya Wilaya ya Namtumbo kwa kuchagua eneo zuri la kujenga Shule ya Sekondari ya Mputa na kuongeza kuwa, ujenzi wake ukikamilika vizuri inaweza kuongezwa hadhi ya kuwa na kidato cha tano na cha sita.

Awali, akitoa taarifa ya ujenzi huo, Mkuu wa Shule hiyo ya Sekondari Mputa, Godlove Chumi amesema ujenzi umefikia asilimia 71 na hadi sasa Sh.

Milioni 379.9 zimetumika kati ya Sh.milioni 560.5 zilizopelekwa kupitia mradi wa SEQUIP kwa ajili ya ujenzi wa shule hiyo mpya.

Habari Zifananazo

2 Comments
Oldest
Newest Most Voted
Inline Feedbacks
View all comments
Back to top button