Serikali kuboresha uendeshaji Amcos

SERIKALI inaenda kufanya maboresho makubwa katika uendeshaji wa  ushirika (AMCOS) ili kuleta tija kwenye ushirika huo.

Akizungumza mkoani Mtwara alipozungumza na wananchi wa kata ya namtumbuka iliyopo Halmashauri ya Mji Nanyamba kupitia mikutano ya hadhara, Mbunge wa Jimbo la Nanyamba Abdallah Chikota amesema tayari baadhi ya mabadiliko ya msingi yameshafanyika katika ushirika huo.

Amesema lengo la maboresho hayo ni pamoja na kuleta ushirika wenye tija unaotatua matatizo ya mkulima.

“Maboresho yajayo inawezekana Amcos zingine zikavunjwa tukawa na Amcos chache zenye tija, sasa hivi Amcos imekuwa mzigo kwa wakulima”

Aidha ametolea mfano changamoto zilizojitokeza katika msimu wa mauzo ya zao la korosho msimu wa mwaka 2024/2025 kwani kumekuwa na upotevu mkubwa wa korosho katika maeneo yao uliyofanywa na baadhi ya viongozi wasiyokuwa waaminifu katika Amcos hizo.

“Na mzigo ule wa mwisho kuathirika ni mkulima ndiyo maana sasa serikali inakuja na mtizamo mwingine, kwahiyo upo uwezekamo katika kata tukawa na Amcos mmoja au mbili zitazoongoza kwa ufanisi mkubwa,”amesema Chikota.

Ameongeza kuwa, “Zitazokuwa na tija na hatikuwa na madhara kwa wakulima vile vile hata uingizaji wa wanachama kutakuwa na maboresho kwani wanachama  watakuwa wengi na maamuzi yatafanywa na wanachama wengi”

Amesisitiza kuwa, lengo ni kuhakikisha kwamba kunakuwa na Amcos bora zenye kujibu kero za wakulima wa zao hilo.

Aidha hayo yamejiri kufuatia moja ya changamoto iliyowasilishwa na baadhi ya wananchi wa kata hiyo  kupitia mikutano ya hadhara iliyofanywa na mbunge huyo kwenye kata hiyo.

Mikutano hiyo ina lengo la kusikiliza changamoto mbalimbali zinazowakabili wananchi hao kwenye maeneo yao lakini kukagua miradi mbalimbali ya maendeleo inayotekelezwa na serikali kwenye kata hiyo na halmashauri kwa ujumla

Habari Zifananazo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button