KUFUATIA changamoto ya athari ya mabadiliko ya tabia nchi maeneo ya Ukanda wa Bahari ya Hindi wilayani Mkinga serikali inatarajiwa kupeleka mradi wa Sh milioni 400 kudhibiti athari za mabadiliko hayo.
Hayo yamesemwa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Dk Ashatu Kijaji wakati wa ziara ya kukagua miradi ya maendeleo pamoja na kuzungumza na wananchi wanaishi kwenye vijiji vinavyopakana na Bahari ya Hindi wilayani Mkinga.
Amesema kuwa wilaya hiyo ni miongoni mwa wilaya zilizoathiriwa na changamoto za mabadiliko ya tabia nchi hivyo Ili kunusuru hali hiyo uwepo wa mradi huo utaweza kumaliza changamoto hiyo lakini na kutoa fursa ya ajira ya Kudumu kwa wananchi wanaoishi maeneo ya pwani ya bahari hiyo.
“Mradi huu unakwenda kudhibiti athari za mabadiliko ya tabia nchi ambayo tayari yameshaanza kuyaona katika maeneo yetu ya bahari Kwa kingo za ardhi kuanza kutafunwa na bahari,”amesema Waziri Dk Kijaji.
SOMA: Serikali kuongeza misitu asili kila halmashauri
Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Dk Batlida Buriani amesema kuwa ushiriki wa wananchi katika kudhibiti uharibifu wa mazingira ikiwemo raslimali za bahari umesaidia zaidi ya wavuvi haramu 100 kusalimisha zana haramu kwenye vyombo vya dola
Waziri Dk Kijaji yupo mkoani Tanga Kwa ziara ya siku mbili ya kukagua miradi ya maendeleo pamoja na mikutano na wananchi waliopo katika wilaya za Tanga, Mkinga Pangani na Muheza.
SOMA: