Serikali kugharamia mazishi waliokufa kwa mafuriko Hanang

MANYARA: RAIS Samia Suluhu Hassan amemuelekeza Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa serikali igharamie mazishi ya waliopoteza maisha kutokana na mafuriko yaliyotokea Wilaya ya Hanang jana.

Maagizo hayo yanaenda sambamba na majeruhi wote kupata matibabu yanayostahili kwa gharama za serikali, huku vyombo vya ulinzi na usalama vikiendelea kutoa msaada wa dharura na uokoaji.

Taarifa iliyotolewa na Mkurugenzi wa Mawasiliano Ikulu imeeleza Rais Samia ameelekeza Serikali ya Mkoa na Kitengo cha Maafa cha Ofisi ya Waziri Mkuu kuhakikisha wananchi wote ambao makazi yao yamesombwa na maji wapate makazi ya muda kwa ajili ya kuwastiri wananchi hao.

Taarifa ya Ikulu imeeleza hadi sasa idadi ya vifo ni 50 huku idadi ya majeruhi waliowasilishwa katika hospitali mbalimbali za mkoa, wilaya na vituo vya afya ni zaidi ya 80.

Taarifa hiyo imefafanua kuwa kaya zilizoharibiwa hadi sasa ni 1,150 idadi ya watu walioathirika ni 5,600 na takribani ekari za mashamba 750 zimeharibiwa.

Habari Zifananazo

Back to top button