Serikali kujenga viwanda vya korosho mtwara

SERIKALI imepanga kujenga kongani ya viwanda vya kubangua korosho katika Mkoa wa Mtwara, ili kuendeleza mnyororo wa thamani wa zao hilo,  Mkurungezi Mkuu wa Bodi ya Korosho nchini (CBT) Alfred Francis amesema.

Mradi huo utagharimu kiasi Sh bilioni 273. Kongani hiyo itajengwa eneo la ekari 1,500 Maranje Halmashauri ya Nanyamba mji, Wilaya ya Mtwara, mkoani hapa.

Francis alisema serikali imeingia ubia na Kampuni ya Arise Integrated Industrial Platforms ambayo inafanya kazi ya kuendesha viwanda vya korosho nchini Benin ili kujenga kongani hiyo.

Amesema kongani hilo litakuwa na uwezo wa kubangua korosho tani 300,000 kwa mwaka na kuzalisha ajira elfu 35.

Kongani litahusisha uzalishaji wa viwanda vya kuongeza thamani ya mazao ya ufuta, kukamua mafuta ya maganda ya korosho.

Francis amesema serikali imeshaanza kufanya tathmini ya ujezi huo, katika ekari 357 ambapo wataanza kujenga hivyo viwanda.

Habari Zifananazo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button