‘Serikali, sekta binafsi zishirikiane kwa manufaa ya vijana

Waziri Mkuu Mstaafu, Mizengo Pinda

DAR ES SALAAM: WAZIRI Mkuu Mstaafu, Mizengo Pinda amesema kuna umuhimu wa kujenga mahusiano mazuri kati ya serikali na sekta binafsi ili kuongeza fursa za ajira kwa vijana.

Mstaafu Pinda ameyasema hayo kwenye Maonesho ya 48 ya Kimataifa ya Biashara (Sabasaba 2024) jijini Dar es Salaam alipotembelea banda la Ofisi ya Waziri Mkuu.

Rais Samia bega kwa bega sekta binafsi

Amesema linapokuja suala la ngazi ya taifa, Rais Samia Suluhu Hassan ndiye huwa Mwenyekiti wa mabaraza yote ili wafanyabiashara waseme shida zao na yeye azipokee na kuzifanyia kazi

Advertisement

“Sekta binafsi zikijikita zaidi kwenye kukuza sekta hiyo na kutafuata ajira. Watu wengi wataishia kwenye sekta binafsi kwa sababu ni eneo kubwa ambalo linaweza kubeba wafanyakazi wengi pengine kuliko serikali,

Sekta binafsi sio tu uchumi lakini ukitafuta ajira, ukikuza sekta hiyo basi watu wengi huishia kwenye sekta binafsi sababu ni eneo kubwa na linaweza kubeba wafanyakazi wengi zaidi pengine kuliko humu serikalini,” amesema Waziri Pinda.

Kwa upande mwingine, Mkuu huyo amepongeza kuanzishwa kwa mfuko wa uwezeshaji, pia amewataka kujithmini kuhusu mfuko huo kwani asilimia kubwa unategemea fedha kutoka serikalini na badala yake waanzishe mfuko mwingine utakaosaidia kuchangia upatikanaji wa fedha na kwenda kutatua changamoto ya ajira kwa vijana.