Serikali: Umeme umefika vijiji 11,973
DODOMA: Serikali imesema vijiji 11,973 sawa na asilimia 97.2 ya vijiji vyote vimefikiwa na huduma ya umme inayotolewa na Wakala wa Umeme Vijijini – REA.
Waziri wa Fedha, Dk Mwigulu Nchemba amesema wakati akiwasilisha Bajeti Kuu ya Serikali kwa Mwaka 2024/25 kuwa vijiji hivyo vina husisha vitongoji 32,827 kati ya 64,359.
Kwa mujibu wa Mwigulu, kazi ya kuunganisha vijiji na vitongoji inaendelea na lengo ni kuhakikisha kila eneo limeunganishwa na huduma hiyo muhimu ya nishati.